We are not currently recruiting Swahili language specialists. We will be recruiting in the future so please bookmark this site and keep checking.
Sayyida Salme alikuwa mwanamke wa mwanzo wa Afrika Mashariki kuandika kitabu na kupigwa chapa katika karne ya 19 Ulaya. Kitabu chake kinaelezea na kuunganisha maisha ya Kizanzibari, Kiarabu na ya Uzunguni. Siku hizi maandishi yake yanatiliwa maanani kwa kuwa watu wanasafiri zaidi na maingiliano yameongezeka.
Maonyesho ya Sayyida Salme kwanza yalifanyika katika ukumbi wa Brunei, London, Aprili 2001. Sasa yanapelekwa Zanzibar na kuoneshwa katika Makumbusho ya Beit el Ajaib kuanzia 14 Julai. Baadaye yatatembezwa katika miji jirani ya mwambao na ya bara ya Afrika Mashariki.
Lengo la maonyesho hayo ni kuwapatia fursa watu mbali mbali kujionea na kuelewa ustadi wa mwandishi huyo mashuhuri katika historia. Pia kutafunguliwa ofisi ya Sayyida Salme katika Mji Mkongwe wa Zanzibar. Kazi yake itakuwa kutekeleza nia yake ya kuchangia maendeleo ya Zanzibar. Hivyo itaendelezaia miradi ya elimu na utamaduni kulingana na mahitaji ya wakati huu. Miradi hiyo itakuwa kama ni chombo cha kuwapatia watu ujuzi wa kazi utakaowaletea maendeleo ya kudumu.
Sayyida Salme alizaliwa 1844 katika Kasri la Mtoni Zanzibar. Ni mtoto wa Mfalme was mwanzo wa Kiomani kutawala Zanzibar kwa mmoja wapo wa wake zake wa kisharkashiya aiyetoka kusini mwa Urusi. Sayyida Salme alikuwa mwanamke wa mwanzo wa kifalme kujifundisha kuandika: jambo ambalo alilifanya kwa kificho kwa kuzinakili hati za Kuran Tukufu na kuaziandika kwenye fupa la ngamia ambalo siku hizo ndio uliokuwa ubao wa kuandikia. Kwani miaka hiyo wanawake wa kifalme wa Zanzibar sana walikuwa wakifundishwa kusoma Kuran, kufanya hesabu, kazi za nyumba na kupewa mawazo ya usimamizi bora wa mashamba yao.
Katika vita vilivyojaribu kumpindua kaka yake ambavyo havikufanikiwa, Sayyida Salme ndiye aliyekuwa akiwaandikia baruwa za siri waasi na kushirikiana na wanawake wenzake kumtorosha mwasi mkuu wa mapinduzi hayo. Mnamo 1866, Sayyida Salme, aliondoka Zanzibar, bila ya kuaga, kuelekea Ujarumani ili kuolewa na Heinrich Reute, mfanya biashara wa Kijarumani aliyekuwa jirani yake Zanzibar. Aliishi Ujarumani na aliwahi kurudi kwao Zanzibar mara mbil, i lakini hakuweza kubaki huko. Alifariki 1924 Ujarumani.
Aliandika vitabu vitatu. Maisha ya Binti Mfalme (1866); kumbukumu aliyoiita Baruwa za Kwetu (1867-80); na Destuti za Syria na matumizi yake (1890). Maisha ya Binti Mfalme ilikuwa ni kitabu cha mwanzo kuandikwa na mwanamke wa Kizanzibari. Kilichotufumbua macho juu ya maisha ya Kifalme ya Zanzibar ambayo hayakujulikana mwanzoni, pamoja na maelezo muhimu ya maisha ya Zanzibar katika Karne ya 19. Baruwa zake ni mfano adimu wa mwanamke asiye mzungu aliyeelezea maisha ya uzunguni ya Karne ya 19. Sayyida Salme alikuwa mwanamke wa mwanzo kufundisha Kiswahili Ujarumani.
Maonyesho yanachangamsha maingiliano ya kitamaduni na ya kibiashara baina ya Zanzibar na nchi za ulaya, yakijaziliwa na masimulizi fasaha ya Sayyida Salme ambayo mara kwa mara yanasisitiza fikra zake katika kuilewa kwetu historia ya Zanzibar. Vielelozo vya kuvutia vilvyotumika katka maonyesho hayo vinamwezesha mtazamaji akutane na Sayyida Salme katika nyakatii tofauti na kuelewa zaidi chanzo cha hadithi yake ya ajabu.
Picha na maelezo yake, vitu vyake binafsi. Mavazi ya kizamani ya Zanzibar, vyombo vya nyumba, vya kuvaa na vyenginevyo vya sanaa vinatoa taswira ya maisha ya kifalme yalivyokuwa Zanzibar, na ya ule wakati wa Sayyida Salme alipoishi Ulaya.
QUESTIONS
1. Where is the Princess Salme exhibition going to be mounted?
2. How did Princess Salme learn to write?
3. What is unusual about Princess Salme's diaries?
4. How will the exhibition fulfil Salme's desire to help Zanzibar?
5. What was remarkable about the work of Princess Salme in Germany?